KUTOKANA na mwezi mtukufu wa Ramadhani, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’ (Pichani) ametengeneza wimbo wa ‘Kaswida’.
Wimbo huo bado hajausambaza katika vituo vya redio, ila unaweza kuusikia kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tunda Man alisema wimbo huo anatarajia kuanza kuusambaza hivi karibuni na kuwaomba mashabiki wake wampe sapoti ya kutosha.
“Kwa kipindi hiki cha Ramadhani, nimeamua kuwapa mashabiki wangu burudani ya dini, hasa ukizingatia na mimi ni Mwislamu niliyelelewa katika maadili ya kidini, hivyo naomba sapoti kwa mashabiki wa kazi zangu,” alisema Tunda Man.
Tunda Man, aliwataka mashabiki na wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula, kwani amepanga kuwapa burudani ya kutosha mara baada ya mfungo wa Ramadhani kumalizika.