![]() |
|
|
|
Mkurugenzi wa uchezaji wa Barcelona Andoni Zubizarreta
amedai kuwa Manchester United wameachana na juhudi zao za kusaka Cesc
Fabregas, kwa mujibu wa ripoti katika vyombo vya habari vya Uhispania.
United, ambao bado hawajanunua mchezaji yeyote mkuu tangu David Moyes amrithi Sir Alex Ferguson kama kocha, tayari wameshuhudia ofa zao mbili za kumtaka mchezaji huyo wa Uhispania zikikataliwa na mabingwa hao wa La Liga.
"Manchester United walikuwa wakimtaka mchezaji huyo, lakini pia wameelewa msimamo wetu ambao ni kwamba hatutamuuza,” golikipa huyo wa zamani wa Uhispania alinukuliwa akisema katika gazeti la Daily Sport linalochapishiwa Barcelona.
"Wamekata tamaa katika juhudi zao za kumtaka.”
Licha ya kujipatia taji lake la kwanza la ligi katika uchezaji wake msimu uliopita, Fabregas amevumilia kipindi kigumu miaka miwili tangu arejee katika klabu hiyo aliyoiacha akiwa na umri wa miaka 16 kujiunga na Arsenal.
Nafasi katika safu ya kati Barca imekuwa nadra na ameumia kutokana na kuwepo kwa wachezaji wenzake wanaochezea pia taifa Xavi, Andres Iniesta na Sergio Busquets, huku jukumu lake la kuwa nyuma ya mshambuliaji mkuu kwa sasa likiwa linashikiliwa na mchezaji bora wa mwaka duniani mara nne Lionel Messi.
Hata hivyo, kutokana na kuuzwa kwa Thiago Alcantara aliyeenda Bayern Munich na ikizingatiwa kwamba Xavi mwenye umri wa miaka 33 anatarajiwa kucheza mechi chache msimu huu, Zubizarreta amesisitiza kuwa Fabregas atakuwa kiungo kikuu kwenye kikosi.
"Cesc ni mchezaji mzuri sana, tunamtegemea. Ana maono, husaidia katika ulinzi, yeye ni Nambari 4 wetu na hatutamuuza.”
Fabregas alifunga mabao mawili alipocheza mara yake ya kwanza msimu huu na kusaidia Catalans kuwalima Santos 8-0 mnamo Ijumaa na pia amesafiri na kikosi kushiriki katika kliniki za kutoa ukufunzi Palestina na Israel kabla ya ziara ya bara Asia.