come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BODI YA LIGI YAFYATA MKIA KWA YANGA, SASA YATANGAZA KUITEMA AZAM TV


Bodi ya Ligi kuu Tanzania  Bara(TPL)  imesema iko tayari kuuweka kando udhamini wa Azam TV endapo itatokea kampuni yenye dau kubwa zaidi.

Bodi hiyo imebainisha kuwa milango iko wazi kwa kampuni nyingine kujitokeza kuchukua nafasi hiyo ambayo Azam imeweka dau la Sh 1.68 bilioni kudhamini.

Ofisa wa bodi hiyo, Silas Mwakibinga aliuambia mtandao huu kuwa milango iko wazi kwa kampuni yoyote yenye dau kubwa kujitokeza kuchukua nafasi ya  Azam TV.

“Ikipatikana kampuni itakayokubali kutoa dau nono zaidi ya lile la Azam TV, bodi iko tayari kuuweka kando udhamini huo wa Azam TV,” alisema Mwakibinga.

Bosi huyo wa bodi ya ligi alibainisha kuwa kampuni hiyo inapaswa kujitokeza ndani ya siku 30 na kusisitiza kuwa milango iko wazi kwa kampuni yoyote ile.

Katika hatua nyingine, Mwakibinga ameeleza kuwa hivi sasa wanajipanga kuhakikisha Ligi Kuu inakuwa ya kisasa sambamba na kuendeshwa bila kuwa na malalamiko kutoka kwa klabu.

“Lengo ni kuhakikisha ligi yetu si masikini tena, kwa kuwa na wafadhili ambao watatufanikisha kuiendesha kisasa zaidi,” alisema Mwakibinga na kuongeza mchakato huo unafanyika kwenye ligi kuu na ligi daraja la kwanza ambayo ndiyo msingi wa kupata wachezaji wazuri wa ligi kuu na timu ya taifa.