MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, M2 the P, (Pichani) ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Masambe Wena’ ambayo ameshirikiana na mkali kutoka kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda.
Kwa mujibu wa mtandao wa DJ Choka, mkali huyo kausambaza wimbo huo katika vituo mbalimbali vya redio wiki iliyopita na tayari umeanza kufanya vizuri.
M 2 the P, alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Wimbo na Jina’ ambao ulimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Msanii huyo aliomba wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwa ajili ya video ya ngoma hiyo, ambayo ana imani itafanya vizuri kutokana na mazingira ambayo atatumia.
Alisema ana imani video ya kazi hiyo itakamilika hivi karibuni na kwamba, amerudi upya katika ‘game’ na wapenzi wake waendelee kumpa sapoti kama walivyokuwa hapo awali.
