come
ROONEY SASA KUTOROKEA KWINGINEKO, AIBWATUKIA MAN UNITED
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ataangalia uwezekano wa kuhamia nje ya England, iwapo hatafanikiwa kuhamia Chelsea majira haya ya joto.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United anatarajiwa kuwasilisha barua ya maombi ya kuondoka wiki hii ili kutilia mkazo wa ofa ya Pauni Milioni 30 kuhamia Stamford Bridge.
United, ambayo inaaminika kutaka kumsajili kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, imeendelea na msimamo wake ikisema hadharani haitamuuza Rooney kwa klabu wapinzani wao wakuu Ligi Kuu England.
Katika kiti cha kuendeshea: Wayne Rooney anataka kuondoka Manchester United majira haya ya joto.
Rooney na Chelsea kwa pamoja wanaendeela kuamini kwamba United na kocha wao mpya, David Moyes watachemsha tu kutokana na jinsi ambavyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aanendelea kutilia mkazo suala la kuondoka baada ya kuitumikia klabu kwa miaka tisa.
Ikiwa hawamruhusu, Rooney ameamua bora kuhamia klabu nyingine itakayomvutia barani Ulaya kuliko kubaki Old Trafford.
Inafahamika kwamba Rooney hahofii kuhamia popote, lakini atafurahi kwenda na mkewe Colleen na wa watoto wao wawili wadogo katika timu ya Ulaya itakayotoa ofa nzuri, ili aondoke Old Trafford.
Hakuwemo katika kikosi cha United kilichokwenda kucheza na AIK Stockholm nchini Sweden jana kujiandaa na msimu, kutokana na maumivu ya bega na Rooney anatarajiwa kupona maumivu hayo aliyoyapata mazoezini mwishoni mwa wiki. Anaweza kuwa tayari kwa safari ya Wembley ambako Moyes atapeleka kikosi chake kwania Ngao ya Jamii dhidi ya Wigan Jumapili.
Marouane Fellaini Marouane Fellaini
Anatakiwa: Marouane Fellaini, akifanya mazoezi na Everton jana, anaweza kuhamia Manchester United