come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BARNABA AANIKA MALI ZAKE MTANDAONI, KUMBE ANAMILIKI NYUMBA YA KIFAHARI.

Mwanamuziki Barnaba aliyepata kutamba na wimbo wake wa Mgubegube amefunguka kupitia ukurasa wake wa facebook na kuachia picha zinazoonyesha mjengo wake wa kisasa kama wafanyavyo nyota wengine wa bongofleva.

Sio kwamba mastaa wa zamani wa bongofleva hawakuwa wanapata chochote kwenye malipo kutokana na kazi zao bali  imefahamika kwamba mipangilio na matumizi mazuri ya fedha havikuzingatiwa sana kwa baadhi ya Wasanii wachache ambao walibahatika kuzipata pesa nyingi zilizotokana na mauzo ya kanda na show.


Wasanii wengi wa bongofleva wa sasa hivi wameshtukia mchezo ndio maana wengi wao wanaingia kwenye headlines za kuonyesha mali zao kama nyumba na magari siku kadhaa tu baada ya kusikika kwenye chati za bongofleva ambapo hii kwa kiasi kikubwa ni kutokana na malipo ya show zao, wengine mauzo ya nyimbo kwenye miito ya simu, dili za makampuni na ishu nyingine.

Barnaba ni miongoni tu mwa waimbaji wenye talent zao na amekua akifanya showz mbalimbali hata nje ya Tanzania pamoja na kupata dili za mashirika/taasisi mbalimbali na kufanya nao kazi zikiwemo za ubalozi mfano Pepsi, Barclays Bank na wengine kama unavyoweza kuona moja ya stori zake za mwaka 2013.