Mapato ya Real ya euro 519 milioni ($704 milioni) yaliweka klabu hiyo mbele ya wapinzani wao wa nyumbani katika mwaka wa kifedha wa 2012/2013, huku mabingwa wa Ulaya Bayern Munich wakijipenyeza nambari tatu mbele ya Manchester United, katika Ligi ya Pesa katika Soka iliyotayarishwa na wahasibu Deloitte.
Paris St Germain (PSG), inayomilikiwa na tajiri kutoka Qatar, na ambapo nahodha wa zamani wa Uingereza David Beckham alimalizia uchezaji wake mwaka uliopita, ilisisitiza kujitokeza kwake kama mwamba katika soka kwa ongezeko la asilimia 81 katika mapato yake hadi karibu euro 400 milioni na kuwa ya tano.
Mapato ya timu 20 za juu yaliongezeka kwa asilimia 8 hadi euro 5.4 bilioni, Deloitte walisema, na kuonyesha kuvutia wka soka kwa watangazaji na wadhamini wanaosaka masoko makubwa ya wateja.
Real Madrid na Barcelona ndizo timu mbili zilizoendeleza ufanisi Ulaya, zikiwa na wachezaji wawili wakuu kama vile Cristiano Ronaldo na Lionel Messi mtawalia.
Klabu hizo mbili zinajivunia nafasi bora ya kifedha ya kuweza kujitetea kivyake katika mikataba ya TV, badala ya kuungana na timu nyingine kuuza haki za TV kama zifanyavyo timu nyingine katika ligi nyingine kuu.
Na licha ya hayo, muundo wa haki za TV wa Uhispania na mgogoro wa kifedha nchini humo umeacha timu ndogo ndogo zikihangaika kifedha na zikitaka kuongezewa pesa kutoka kwa watangazaji.
TIMU 20 BORA KATIKA LIGI YA PESA KATIKA SOKA- Mapato ya 2012-13 (euro milioni)
1. Real Madrid (Uhispania) 519
2. Barcelona (Uhispania) 483
3. Bayern Munich (Ujerumani) 431
4. Manchester United (Uingereza) 424
5. Paris St Germain (Ufaransa) 399
6. Manchester City (Uingereza 316
7. Chelsea (Uingereza 303
8. Arsenal (Uingereza) 284
9. Juventus (Italia) 272
10. AC Milan (Italia) 264
11. Borussia Dortmund (Ujerumani) 256
12. Liverpool (Uingereza) 241
13. Schalke 04 (Ujerumani) 198
14. Tottenham Hotspur (Uingereza) 172
15. Inter Milan (Italia) 169
16. Galatasaray (Uturuki) 157
17. Hamburg SV (Ujerumani) 135
18. Fenerbahce (Uturuki) 126
19. As Roma (Italia) 124
20. Atletico Madrid (Uhispania) 120