BABA mzazi wa Balotelli wa Tanzania amefariki leo katika ajali ya gari iliyotokea Buguruni jijini Dar es Salaam jioni hii ya leo, kwa mujibu wa Salum Mfunga ambaye ni afisa habari wa umoja wa watuma salamu Dar es Salaam na Pwani amesema kuwa baba mzazi wa mtoto huyo ambaye amefanana na staa wa AC Milan ya Italia Mario Balotelli pia amekuwa akimuiga kwa unyoaji wake wa nywele.
Taarifa hizo zinasema kuwa mazishi yatafanyika kesho saa tisa alasiri katika makaburi ya Tabata Segerea na msiba upo Ubungo jirani na Tanesco, Baba Balotelli si maarufu sana kama ilivyo kwa mwanaye au mkewe anayefahamika kwa majina ya Beatrice wa Kariakoo au Mama Balotelli wa Tz.
Umaarufu huo umekuja baada ya mtoto wao Balotelli wa Tz kufanana na staa huyo wa AC Milan, pia unyoaji wake wa nywele nao ni gumzo kubwa, mungu ailaze roho ya baba mzazi wa Balotelli wa Tanzania Amina.
