MABAO mawili ya Jordan Henderson na mawili ya Daniel Sturridge yameipa Liverpool ushindi wa 4-3 dhidi ya Swansea katika mchezo mgumu wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Anfield.
Kikosi cha Brendan Rodgers kimeendelea kuwanyatia vinara wa ligi, Chelsea sasa wakizidiwa kwa pointi nne tu.
Mabao ya Swansea yalifungwa na Jonjo Shelvey moja na mawili Wilfried Bony. Liverpool inatimiza pointi 56 baada ya kucheza mechi 27, ikiendelea
kutulia nafasi ya nne, nyuma ya Manchester City pointi 57 mechi mechi 26, Arsenal pointi 59 mechi 27 na Chelsea pointi 60 mechi 27.
