
Rais wa Ukraine aliyeondolewa madarakani Victor Yanukovych amefunguliwa mashtaka
Ukraine imetoa hati ya kukamatwa
kwa Rais aliyeondolewa madarakani, Victor Yanukovych, Waziri wa mambo
ya ndani wa mpito ametangaza hatua hiyo.
Wabunge walipiga kura kumuondoa Yanukovych siku ya jumamosi baada ya maandamano ya miezi kadhaa yaliyojitokeza baada ya kupinga kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Machafuko yaliyotokana na maandamano hayo yalisababisha watu kadhaa kupoteza maisha juma lililopita.
Avakov amesema Yanukovych alionekana mjini Balaklava siku ya jumapili, lakini mpaka sasa hajulikani mahali alipo.