come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MGAMBO YAAPA KULIPIZA KISASI KWA SIMBA LEO.

Na Regina Mkonde

MGAMBO JKT ya Tanga leo jioni inashuka katika uwanja wa CCM Mkwakwani kuivaa Simba ya Dar es Salaam katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, Simba ambayo ina kumbukumbu ya kuifunga Mgambo mabao 6-0 katika mzunguko wa kwanza kwa vyovyote leoitakutana na ushindani mkubwa.

Simba ambayo ilitoka sare ya kufungana na 1-1 na Mtibwa Sugar Jumatano iliyopita itakuwa na kazi ngumu pale vijana wa Mgambo JKT watakapotaka kulipiza kisasi, vijana wa Mgambo wamepania vilivyo kushinda mechi ya leo lakini Simba ni timu kubwa yenye mikakati ya ushindi kila mechi.

Kocha wa Simba Mcroatia Zdravko Logarusic ametamba kuzoa pointi tatu katika mchezo huo, lakini vijana wa Mgambo wamesema haiwezekani lazima wachomoze na ushindi katika uwanja wao wa nyumbani, Simba haina rekodi ya kushinda katika uwanja wa Mkwakwani inapokutana na timu hiyo na mara ya mwisho zilikutana msimu uliopita ambapo zilitoka suluhu .