come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA INAWEZA BILA OKWI.

Na Regina Mkonde

MASHABIKI tofauti wa vilabu vya mpira wamejiuliza maswali mengi juu ya ushindi walioupata Yanga juzi, dhidi ya timu ya Comoro (Komorozine) na kuacha wapinzani wengi na kihoro juu ya ushindi huo.


Mi najua hizo ni mbwembwe tu za Yanga maana kutangulia kwenda si kuwahi kufika alisema mpinzani mmoja(jina limehifadhiwa) na kudai kuwa Yanga iliionea comorizine sababu haiko vizuri,na kusema kuwa wapinzani wanataka wacheze na timu kali kama Simba sc,Azam Fc n.k ndipo itakapojulikana kama Yanga jembe au mbwembwe tuWengine wakadai kuwa Yanga haina soko sababu ya nyota wao Emmanuel Okwi kuzuiliwa kwa muda kuichezea timu hiyo kutokana na utata uliotokea TFF juu ya usajili wake, hivyo Yanga ikimkosa Mganda huyo machachari Okwi hawataweza kuchukua ushindi endapo itapambana na timu kali kama Simba Sc, Azam Fc nk. Bali watazidi kuzionea timu vibonde tu, walisema baadhi ya wapinzani wao.

Hata kama imeifunga Komorozine mabao 7-0, wala hawatutishi, bali tunawasubiri kwa hamu mechi ifike ili tuzidi kuwaonyesha kwamba sisi bado mtani jembe, ushindi wao wa juzi ni mbwembwe tu lazima tutawafunga maana hawana ujanja kwetu.Alisema Jumanne mkazi wa Manzese Dsm.

Kulingana na vitisho vyote hivyo Wanayanga nao hawakubaki nyuma na kusema kuwa ushindi upo pale pale hata kama Straika wetu Emmanuel Okwi amebaniwa kuingia uwanjani kwa muda, tutazidi kuongeza makamuzi mpaka tuchukue ubingwa, alisema shabiki mmoja wa Yanga aliyejitambulisha kwa jina moja la Bw Athmani