come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SIRI YAFICHUKA MAZISHI YA BABA BALOTELLI.

Na Salum Fikiri Jr

SIKU moja mara baada ya Mtandao huu kutangaza kifo cha baba mzazi wa Balotelli wa Tanzania anayefahamika kwa jina  Tonny, siri kubwa imegunduliwa katika msiba wake ambapo Staa wa Leo imezipata,siri hiyo ni ya mfiwa Mama Balotelli wa Tanzania ambaye aliitoa moyoni.

Akizungumza mara baada ya mazishi ya marehemu mchumba wake, Beatrice Shadrack maarufu Beatrice wa Kariakoo ama Mama Balotelli wa Tanzania kama anavyofahamika kutokana na mwanaye mwenye miaka miwili kufanna na nyota huyo wa AC Milan.

Mama Balotelli ametoboa siri hiyo kuwa alitaka kufunga ndoa na marehemu mchu8mba wake siku si nyingi mwaka huu, wakiwa wanatoka matembezini maeneo ya Buguruni marehemu aligongwa na gari lililoacha njia na kumparamia hatimaye kusababisha mauti yake.

Mama Balotelli alisikitika sana kufuatia kifo hicho na kumwacha katika majonzi makubwa katika kipindi hiki kigumu, aidha alifafanua kuwa marehemu hakuwa baba mzazi wa mwanaye Balotelli tofauti kama ilivyoandikwa hapo awali,anadai kuwa marehemu alikuwa katika harakati za kuoana lakini mipango ya mungu ilikataa.


Jana mazishi ya mchumba huyo wa Mama Balotelli yalifanyika katika makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji hili na mikoa jirani, enzi za uhai wake marehemu alikuwa kiongozi wa Jumuiya ya vijana ya Uvccm ambapo jana  itifaki ya kichama ilizingatiwa.