Mshambuliaji
huyo wa Liverpool alihitaji upasuaji wa goti lake, na kuwapa hofu
wanananchi wa Uruguay kama tegemeo lao hilo litamudu kucheza Kombe la
Dunia.
Lakini katika ujumbe wa video aliourekodi, Suarez amesema yuko njiani kupona.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 alionekana yuko vizuri wakati akifanya
mazoezi na Uruguay nje ya kambi ya timu yao mjini Belo Horizonte jana.
Daktari wa misuli wa timu, Walter Ferreira akimfuatilia Suarez
Anakimbizana na muda: Suarez anatumai kuwa fiti kuichezea Uruguay mchezo wa fungi dhidi ya Costa Rica Juni 14
"Mguu unaendelea vizuri,"amesema Suarez. "najisikia vizuri sana. Nahitaji siku hadi siku, lakini kila kitu kinakwenda vizuri,".
"Nataka kuwashukuru wote kwa sapoti yenu mnayonipa katika wiki hii na sasa fikra zangu zipo kwenye Kombe la Dunia.'
Uruguay
wataanza kampeni yao dhidi ya Costa Rica Jumamosi, saa kadhaa kabla ya
mechi nyingine ya Kundi D baina ya England na Italia mjini Manaus.
Uruguay mazoezini jana
Suarez
alifanya mazoezi tofauti na wachezaji wenzake, akipiga mashuti mepesi
na kujaribu kutoa pasi laini kwa mguu wake wa kushoto- huku watu watatu
wa daktari la tiba la timu hiyo wakimfuatilia. Wakati wachezaji wenzake
wakicheza meci mazoezi, Suarez alikuwa pembeni ya Uwanja.
Suarez anaweza kupumzishwa katika mechi ya kwanza, ili arejee kutoa mchango wake katika mechi ngumu dhidi ya England na Italia. Timu hiyo ya Amerika Kusini iliyofika Nusu Fainali miaka minne iliyopita, iliwasili Belo Horizonte juzi.