|
|
Hatimaye, mshambuliaji matata, Diego Costa, sasa
ni mchezaji wa miamba wa Uingereza, Chelsea, baada ya klabu hicho
kutangaza wamekamilish uhamisho wake kutoka Atletico Madrid.
Taarifa hiyo iliyochipuka Jumanne inasitisha kipindi cha miezi kadhaa ambacho mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil anayechezea Uhispania amehusishwa na kudunga hema ugani Stamford Bridge.
Chelsea walisema wamelipa kipengee cha kumnunua kwenye kandarasi yake na mabingwa hao wa La Liga na makubaliano yameafikiwa na mchezaji mwenyewe aliyeshindwa kuwika kwenye Kombe la Dunia ambapo mabingwa Uhispania waliondolewa awamu ya makundi.
“Klabu cha kandanda cha Chelsea kinadhibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa na Atletico Madrid kwa uhamisho wa Diego Costa. Chelsea wametimiza matakwa ya kumnunua na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania,” taarifa kwenye tovuti lao rasmi ilisema.
Mwalimu wa Chelsea, Jose Mourinho, amekuwa kwenye harakati ya kufanyia safu yake ya mashambulizi baada ya kushuhudia Fernando Torres, Demba Ba na Samuel Eto'o wakifunga magoli 26 pekee kwenye mashindano yote walioshiriki musimu jana.