MSHAMBULIAJI Robin van Persie aliondoka kwenye mazoezi ya timu yake ya taifa, Uholanzi baada ya saa moja ya kujifua vikali mjini akiwa amefungwa plasta mguuni mjini Rio leo.Nyota huyo wa Manchester United, ambaye amebeba matumaini ya kocha Louis van Gaal kutwaa Kombe la Dunia, alikuwa amefungwa plasta ya kutosha katika mguu wake wa kushoto wakati wakiondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Flamengo.
Uholanzi inamenyana na Costa Rica mjini Salvador katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia Jumamosi na inamuhitaji van Persie kuwa fiti.

