come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAJERUHI WANAITESA ARSENAL

Aaron Ramsey

Mwalimu wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema klabu chake kiko kati ya mgogoro wa majeraha huku wakijiandaa kucheza na Galatasaray katika ligi ya mabingwa Ulaya kabla ya kutembelea viongozi wa ligi ya Premier ya Uingereza, Chelsea.

Arsenal walitoka kutoka nyuma na kutoka sare ya 1-1 dhidi ya watanashari wao, Tottenham Hotspurs ambao ni majirani London kaskazini kwenye kivumbi ambacho Alex Oxlade-Chamberlain alifyatua goli la kusawazisha.
Lakini Wenger alibaki na zogo kichwani pale viungo Mikel Arteta na nyota Aaron Ramsey walilazimika kutoka uwanjani kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na majeraha ya shavu la mguu na ukano wa mvungu wa goti.

Wawili hawa watakosa mechi mbili zinazofuata huku wasiwasi kuhusu kiungo mwingine, Jack Wilshere, ambaye aliumia kifundo cha mguu katika mechi hiyo ukiendelea.


“Ghafla, tumejipata bila wachezaji wa kutosha kwani leo tulipoteza watatu ikikumbukwa ya kwamba wawili (Olivier Giroud na Mathieu Debuchy) watabakia nje kwa muda mrefu na ukiongeza Theo Walcott, wamekuwa sita.

“Abou Diaby hayuko tayari na hapo kuna hofu kubwa,” mwalimu huyo alisema.