come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NEYMAR, MESSI WAING'ARISHA BARCELONA

Neymar & Leo Messi 

Kocha mkuu wa Barcelona, Luis Enrique, amemiminia washambuliaji nyota, Lionel Messi na Neymar baada ya wawili wao kufunga walipoadhibu vikali Levante 5-0 Jumapili.

Ijapokuwa Messi alitupa penalti katika kipindi cha kwanza, Barca waliendeleza mwanzo mwema katika ligi ya La Liga wakati staa huyo wa Argentina alipounganishia Neymar na Sandro Ramirez kupachika wavuni kabla ya kufunga udhia dakika 18 kabla ya muda wa kawaida kukatika na goli lake.

Ilikuwa ni mara ya sita ndani ya mechi tano kwa Messi kuandalia wenzake nafasi ya kufunga na ukakamavu wake kulizuzua kocha wake.

“Leo Messi ni mchezaji wa kikee na spesheli. Wenzake wanafahamu vizuri kwamba wakati ana mpira, anaweza kuwaunganishia visafi juu ya kuchenga wapinzani wake.


“Nafurahia kuwa wenzake wamegundua hali hii wenyewe na wamechukua fursa za kufaidika na ubora wa Leo. Katika mechi hii, aliadaa mabao kadhaa kwa njia ya kuvutia na alifunga lake mwenyewe katika mchezo kamili,” Enrique alisema.

Bao la Neymar lilikuwa picha ya alilofunga Athletic Bilbao wiki jana katika ushindi wa 2-0 baada ya kasi yake kulemea mabeki wa Levante huku Messi akimpata na mpira juu juu kumpatia fursa ya kutia kizimbani.

“Ana uwezo wa kupokea mpira na mguu na kushambulia mianya iliyowachwa wazi. Kila mshambuliaji ni lazima atafute kila aina ya uwezo na sio Neymar pekee, Sandro na Pedro na Leo waliweza kushamiri katika mashambulizi,” Enrique aliongeza.