come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

OZIL AWAPUUZA WANAMKOSOA

Mesut Ozil 

Nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil, amejibu kwa kejeli shutuma zinazoendelea kuhusu kandanda yake na timu yake ya Uingereza, Arsenal muhula huu.
Wengi wamejitokeza kukashifu mchezo wake tangu kuhamia Arsenal kwa rekodi yao ya pauni milioni 42 za Uingereza kutoka Real Madrid Septemba mwaka uliopita.

Mashabiki wengi wa Arsenal wamegadhabika na mchango wako musimu huu lakini alionyesha umaahiri wake wikendi jana alipofunga bao na kuunganisha lingine kwenye ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Aston Villa.

Ingawa anahisi shutuma dhidi yake hazina haki, amekubali kuwa amezoez hali hiyo alipokuwa anachezea Schalke, Werder Bremen na Real.


“Sichezi ili kudhihirisha chochote kwa mtu yeyote, nachezea Arsenal. Nahisi nashutumiwa zaidi kuliko wengine kama vile ilivyokuwa Bundesliga na Real Madrid,” Ozil aliambia wanahabari wa Ujerumani, dpa.
“Majuma 10 yaliopita, nilichaguliwa kwa kikosi cha ligi ya Uingereza na mashabiki kupitia mtandao na nilikuwa bingwa wa dunia wakati huo.

“Tumeanza musimu juzi na tuna wachezaji wapya kwenye nafasi muhimu. Huu ni mchezo wa umoja wa kikosi na ninawajibika kujiweka katika kiwango sawa na wenzangu.”

“Baada ya mapumziko ya kiangazi na mechi chache za musimu, maswali yameibuka tena na hilo si jambo la kawaida na sijui naweza patiana nini,” nyota huyo aliongeza.