come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DEBUCHY NJE MIEZI MITATU

Mathieu Debuchy

Arsenal watakosa huduma za beki wao wa kulia, Mathieu Debuchy, kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu.

Mchezaji huyo wa kitaifa wa Ufaransa alijiunga na Arsenal Julai kwa ada inayoaminika kuwa pauni milioni 12 za Uingereza lakini baada ya mwanzo mwema na timu yake mpya, aliumia kwenye sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa Manchester City mapema mwezi huu katika mechi ya ligi ya Premier.

Awali, Arsenal walikita matumaini Debuchy aliteguka lakini mitihani iliyofanywa baadaye ilionesha mishipa imekatika.

“Alikuwa na upasuaji ijumaa na atakosa mchezo kwa miezi mitatu. Yote yalienda sawa na anaweza rudi majuma mawili mbele au majuma mawili nyuma wa kipindi hicho cha miezi mitatu,” mwalimu wake, Arsene Wenger, alitangaza.


“Ni pigo kwetu lakini ukubwa wake utabainika baadaye kwani italingana na vile kutaziba nafasi yake. Tulinunua (Calum) Chambers kutekeleza hilo.”