Samatta
ashindwa kufikia rekodi ya Mputu
Timu Entente Setif ya Algeria sasa
itapambana na AS Vita Club ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika fainali
ya Klabu Bigwa barani Afrika baada ya kuiondoa TP Mazembe pia ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kwa faida ya magoli ya ugenini japo TP Mazembe ilishinda
hapo jana mechi ya nusu fainali kwa magoli 3 - 2.
Entete Setif na TP Mazembe zote
zilimaliza nusu fainali kila moja ikiwa na magoli manne kwa manne,magoli mawili
Setif iliyoyafunga ugenini imewasaidia kuwa timu iliyofunga magoli mengi ikiwa
ugenini.
Nayo AS Vita Club imetinga hatua
hiyo fainali baada ya kuibamiza CS Sfaxien ya Tunisia siku ya jumamosi kwa
ushindi wa jumla wa magoli 4 - 2.
Hata hivyo mashabiki TP Mazembe
pamoja na timu yao kutolewa katika mashindano hayo ambayo sasa itachezea mechi ya
kutafuta mshindi wa tatu wamesema wataiunga mkono AS Vita Club ambayo ni timu
nyingine kutoka DRC.