come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

VAN PERSIE ASIFU WASHAMBULIAJI WENZAKE MAN UNITED, ADAI INAWAPA HOFU WAPINZANI WAO

Robin van Persie 

Robin Van Persie anaamini kwa dhati kuwa washambulizi ghali walioletwa Manchester United wana uwezo wa kutia wapinzani wao hofu kubwa.

Meneja wa United amesajili Radamel Falcao na Angel di Maria kukamilisha kitengo kikali cha mashambulizi kinacho husisha straika huyo nyota wa Uholanzi na kigogo mwenzake wa Uingereza, Wayne Rooney.

Wanne hao ni ndoto ya wengi lakini United wamejipata taabani kwasababu ya ngome legevu ambayo imetoboka magoli 13 kwenye mechi saba msimu huu.
Van Persie aliinuliwa moyo na ushindi wao wa 2-1 dhidi ya West Ham wikendi iliyopita licha ya kumaliza na wachezaji 10 baada ya nahodha Rooney kuamrishwa nje ya uwanja kufuatia mchezo mbaya ambao umefanya akapigwa marufuku ya mechi tatu.


“Tunauwezo wa kutia wengi hofu na mechi kama ushindi wetu wa 4-0 dhidi ya QPR ni dhihirisho ingawa tuliteleza wakati tulipoteza 5-3 kwa Leicester.

“Jinsi tulivyoshinda wikendi iliyopita ni ujumbe kwamba hata katika mechi ngumu, tuna uwezo wa kuzoa ushindi na letu ni kufuatilia hilo na mwelekeo unaofaa. Nyakati nyingine wasiwasi ulitanda lakini tulistahimili mashabulizi na kufanikiwa mwishowe,” Van Persie alisema.

Straika huyo anayefahamu Van Gaal kutoka huduma yake na kikosi cha kitaifa cha Uholanzi aliongeza dhamiria ya kumaliza miongoni mwa nne bora ingali ipo huku United wakisaka kujiinua kutoka janga la kumaliza wa saba muhula jana na kufuzu tena shindano la ligi ya mabingwa ya Ulaya.