come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DUNGA AKANUSHA KUIBEZA ARGENTINA

Dunga 

Kocha wa Brazil Dunga amekanusha vikali ripoti kuwa aliwabeza Argentina kama watumizi wa dawa ya kulevya baada ya kunaswa picha akichuna pua yake na kuashiria kitengo cha ufundi cha watanashari wao Jumamosi.

Dunga aliongoza Brazil kuwachakaza Argentina 2-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyojaa uhasama jijini Beijing alipofanya ishara hiyo inayohusishwa na watumizi wa dawa ya kulevya ya cocaine.

Akizungumza kuhusu tukio hilo Singapore Jumatatu, mwalimu huyo alisema alikuwa analalamikia mchafuko wa hewa kwenye jiji hilo kuu la Uchina ambao uliziba mapua ya wachezaji wake kwa uvundo.

“Sikutaja wachezaji ni watumizi wa madawa ya kulevya, taarifa hiyo ilitoka kwa waahabari. Pengine mchafuko wa hewa ulichangia wachezaji wengi kubanwa mapua,” Dunga aliambia wanahabari Singapore ambapo watachuana na miamba wa Asia, Japan Jumanne.


Wanahabari walichambua ishara yake kuashiria utumizi wa mihadarati miongoni mwa wachezaji wa Argentina huku ikikumbukwa kuwa nyota wao wa zamani, Diego Maradona, alikuwa na matatizo makubwa na cocaine.