come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

AC MILAN ITAREJEA KWENYE MAKALI YAKE KAMA ZAMANI



Mumiliki wa vigogo wa ligi kuu ya Italia, Serie A AC Milan, Silvio Berlusconi ana imani kuwa watarejelea utukufu wao wa zamani nchini humo na Ulaya chini ya utawala wa kocha mkuu mpya na gwiji wao wa zamani, Filippo Inzaghi.

“Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya itakuwa Milan 2016. Hakuna linalotuzuia kuota tutaishiriki,” Berlusconi ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo aliambia gazeti la Gazzeta dello Sport Jumatatu.
Inzaghi aliyemrithi kiungo mashuhuri wa zamani,

 Clarence Seedorf, alishinda mataji mawila ya Serie A na mawili ya Ligi ya Mabingwa akiwa mshambuliaji nyota alipowachezea kutoka 2001-2012.

Wana Rossoneri kama klabu hicho kinacho fahamika kote duniani wamejipata wakishuka hadhi kutokana na matatizo ya kiuchumi yaliokumba Italia miaka chache iliyopita.


Ingawa walinyakua taji la Serie A la 2011, Milan walijipata walala hoi baada ya wachezaji wao mashuhuri kuwatoroka kutafuta donge nono kwingineko.

“Ni muhimu kukumbuka tunazidi kulipa mishahara ya kiwango kikuuu na mwaka huu, ni lazima tuwekeze euro milioni 65 ili kustawisha timu hii,” Berlusconi aliongeza baada ya AC Milan kushindwa kufuzu mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane Serie A musimu uliopita.

Tangu kumiliki timu hiyo Februari 1986, Berlusconi amewezesha kipindi cha ufanisi mkubwa kwenye historia yao kwa kusaini wachezaji mashuhuri duniani.