Kocha mkuu wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo ametamba kuibuka na ushindi dhidi ya Simba watakapokutana Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa ligi kuu mkondo wa kwanza, Maximo ambaye jana aliingiza kambini timu yake Kunduchi Beach amejitamba kushinda mchezo huo.
Akizungumza na Staa wa Leo, Maximo ametamba kuwa Yanga iko vizuri kuliko Simba na atayari ameshajua dawa ya kuwadhibiti nyota wa Simba hasa Emmanuel Okwi, Shaaban Kisiga na Haruna Chanongo, 'Yanga iko vizuri kila eneo imetimia ni lazima Simba ifungwe', alitamba Maximo.
Mbrazil huyo ametambia nyota wake wakali Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho, Geilson Santana Jaja na Haruna Niyonzima, ambapo pia ametambia mabeki wake Nadir Haroub 'Cannavaro', Mbuyu Twite, Kelvin Yondani,. Juma Abdul na Oscar Joshua au Edward Charles Manyama.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars ameendelea kukimwagia sifa kikosi chake na kudai ushindi ni lazima, 'Simba haiwezi kutufunga hata kwa dawa, hawana timu ya ushindi wakijitahidi sana labda droo, lakini lengo langu ni kuibuka na ushindi, kambi yao ya Afrika Kusini hainitishi kwani uchovu wa safari tu utapelekea kipigo kwao', aliongeza Mbrazil huyo mwenye misimamo