![]() |
|
|
|
Kocha wa mabingwa wa Afrika Nigeria Stephen Keshi
huenda akatimuliwa mamlakani kufuatia kuongezeka kwa shinikizo la wengi
nchini humo wanaotofautiana na jinsi anakufunzi miamba hao.
Nigeria wamo hatarini ya kutoshiriki Kombe la Maitafa Bara ya Afrika (Afcon) mwaka ujao kwani wanavuta mkia Kundi D la raundi ya mwisho ya kufuzu na alama moja pekee baada ya kushindwa kwa mshtuko na Sudan 1-0 wikendi iliyopita.
Wana Super Eagles ambao walishinda taji hilo 2013 watawaalika Sundan jijini Abuja Jumatano kabla ya kusafiri mwezi ujao kuchuana na Congo Brazzaville walio nafasi ya pili ambao waliwanyuka 3-2 nyumbani huku Afrika Kusini wanaoongoza kundi hilo
kuwatembelea kufunga ratiba ya mechi zao za kufuzu.
Magwiji hao hawana linguine ila kushinda mechi zao zilizosalia na kuomba matokeo kwingineko yatawafaidi ili kupata nafasi ya kusakata kandanda nchini Morocco kwenye fainali za kombe hilo Januari.
Huku akiomba msamaha kwa kushindwa na Sudan, Keshi amedai kuwepo kwa njama ya kuhakikisha atafeli.
“Kuna watu ambao sitataja ambao nia yao ni kuhakikisha hatufanikiwi na wanataka kusambaratisha timu hii. Watu wengine wanataka kusaliti taifa ili walainishe mifuko yao na pesa. Wanataka kuangusha Super Eagles.
“Ni aibu hawataki Super Eagles wafuzu Afcon, wanataka tuondolewe mara moja lakini hao si Jalali,” Keshi alilalamika.
Mashabiki waliosubiri kikosi hicho waliwafokea kwenye uwanja wa ndege wa Abuja huku hatima ya Keshi ikitawala vichwa vya habari nchini humo yenye wafuasi sugu wa soka.
“Keshi ni kocha wa kulipwa na uhakika ni kwamba akimaliza kibarua hiki, atapata kazi nyingine bila wasiwasi,” mwalimu huyo ambaye anatumikia bila kandarasi baada ya makubaliano yake na shirikisho la kandanda Nigeria kuisha Julai baada ya Kombe la Dunia nchini Brazil alizidi.