Mchunguzi
 mkuu wa maadili katika shirikisho la soka duniani FIFA, amesema 
shirikisho hilo linapaswa kuonyesha uwazi kuhusu linavyoendesha shughuli
 zake.
Mchunguzi huyo ambaye pia ni wakili mjini New York, Michael
 Garcia, ameandika ripoti kuhusu uchunguzi unaohusiana na madai ya 
ufisadi katika mchakato wa kura ya nchi itakayoandaa michuano ya kombe 
ya dunia mwaka 2018 na 2022.
Lakini FIFA haiko tayari kuchapisha ripoti hiyo kuambatana na masharti na sheria zake kuhusu siri za shirikisho hilo.
Michael Garcia anataka FIFA kubadilisha mfumo unaotumiwa kuendesha shughuli zake hasa kuhusiana na maswala yenye usiri mkubwa.
Shirikisho hilo limekataa kufichua uchunguzi wake kuhusu madai ya ufisadi.
Lakini akiongea mjini London, alisema shirikisho hilo halina uwazi katika mipango yake jambo ambalo ni muhimu sana kwa shirikisho la kimataifa licha ya kutambua ugumu wake
.
Alielezea namna ambavyo shirikisho la kimataifa la Olimpiki, lilichukua hatua na kuchapisha matokeo ya uchunguzi katika sakata ya rushwa ya Salt Lake City.
Na katika kauli yake kali kumhusu Rais wa shirikisho la FIFA, Sepp Blatter Bwana Garcia alisema mageusi ya ukweli yanatoka kwa uongozi mzuri ambao unaweza kubadilisha mienendo ya shirikisho hilo.