come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YONDANI, CANNAVARO FITI KUIVAA SIMBA JUMAMOSI

Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha uvumi ulioenea kuwa nyota wake wawili Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub Ally 'Cannavaro' ni majeruhi na hawataitumikia Yanga itakapokutana na Simba siku ya Jumamosi.

Cannavaro ambaye aliumia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa akiitumikia timu ya taifa Taifa Stars mwishoni mwa wiki ilipocheza na timu ya taifa ya Benin kwenye uwanja wa Taifa na Stars kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Daktari wa Yanga Juma Sufiani ameuambia mtandao huu kuwa mabeki hao wa Yanga na timu ya taifa wapo fiti na wataiongoza Yanga kuivaa Simba katika mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya watani zao Simba ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka hapa nchini.


Hofu ilianza jana wakati wachezaji hao waliposhindwa kuendelea na mazoezi na wenzao na kujikuta wakikaa benchi kuungana na mashabiki kutokana na majeraha yaliyokuwa yakiwasumbua, Cannavaro aliumia akiwa katia majukumu ya timu ya taifa, wakati Yondani alikuwa akiugulia tu.

Yanga iliingia kambini Jumatatu katika hoteli ya Landmark iliyopo Kunduchi Beach huku ikijifua katika uwanja wa Boko Veteran ambao pia ulikuwa ukitumiwa na mahasimu zao Simba ambao kwa sasa wameweka kambi yao nchini Afrika Kusini.

Miamba hiyo inashuka dimbani Jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa huku kila moja ikiwa imecheza mechi tatu, Yanga imefikisha pointi sita baada ya kucheza mechi tatu ambapo ilianza kucheza na Mtibwa Sugar na kulala 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, lakini ikazinduka kwa kuzilaza Prisons ya Mbeya 2-1 na JKT Ruvu ya Pwani 2-1.

Wakati watani zao Simba yenyewe imecheza mechi tatu zote kwenye uwanja wa Taifa na kuambulia sare mfululizo, Simba ilianza kucheza na Coastal Union ambapo zilifungana 2-2, kisha ikacheza na Polisi Moro na kufungana 1-1 baadaye Stand Unite ya Shinyanga 1-1/