MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Brazil Geilson Santos Santana 'Jaja' ametamba kuwatungua Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Oktoba 18 mwaka huu.
Akizungumza na Staa wa Leo, Jaja amesema Simba ni timu ya kawaida lakini ni kubwa na ina presha, amedai mechi hiyo itampa nguvu na kufanya acheze kwa uchangamfu mkubwa na kuweza kuonyesha mambo yake kama alivyofanya dhidi ya Azam FC ambapo alifunga magoli mawili.
Katika mchezo huo Yanga iliwafunga Azam FC mabao 3-0 na kutwaa Ngao ya jamii, ushindi wa Yanga dhidi ya Azam ulidhihirisha uwezo wa straika huyo wa Kibrazil ambaye alianza kukosolewa na mashabiki wa soka wakiwemo wa Yanga.
Jaja amesema anajisikia furaha anapocheza kwenye mechi iliyojaza mashabiki wengi, aliongeza kuwa hofu ya watu wengi ndio inampa changamoto na kujikuta anafanya mambo makubwa uwanjani, amesema Simba ni timu inayompa ahueni ya kufunga kwani anawaamini viungo Mrisho Ngassa, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima na Simon Msuva ambao watamngenezea nafasi nyingi za kufunga.
Tangia kuanza kwa ligi kuu bara, Jaja ajafunga hata bao moja lakini hii yote inatokana na kukamiwa na mabeki wa timu pinzani, Yanga imecheza mechi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Yanga ililala 2-0 kisha ikazinduka na kuzifunga Prisons ya Mbeya 2-1 na JKR Ruvu ya Pwani pia 2-1.
Lakini katika mechi hizo zote Jaja ameshindwa kutoka na bao ingawa alipata nafasi ya kufunga walipocheza na Mtbwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Yanga ilipata penalti na alipiga Jaja na kupoteza, hata hivyo mwamuzi alilikataa goli zuri lililofungwa na Jaja.
Na katika mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita kati ya Yanga na JKT Ruvu ambapo Yanga ilishinda 2-1, Jaja alionyesha kiwango cha hali ya juu mpaka kumtisha kocha mkuu wa Simba Mzambia Patrick Phiri, Jaja alionyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho zilizopekelea Yanga kupata mabao