come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LAMPARD ANOGEWA NA MAN CITY

Frank Lampard 

Frank Lampard amekiri kwamba ana jukumu la kuendeleza mchezo wa hali ya juu ili aongezewe muda na mabingwa wa Premier, Manchester City.

Mkopo wake kutoka klabu cha Marekani New York City FC utaisha mwakani wakati ligi ya nchi hiyo MLS itangoa nanga.

Lampard ambaye amefunga magoli manne katika mechi sita alichochezea City ananuia kuendeleza matokeo hayo ngoma baada ya nyingine.


“Niko hapa hadi Januari 1 na nitatilia hilo makini nikisubiri kutizama yatakayojili lakini kikao change hapa kinalingana na mchezo wangu na ikiwa sitacheza vyema, watanitimua hapa,” Lampard alisema.