come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

USHINDI WA JUVE WAZUA UTATA ITALIA



Uvundo wa sakata umetanda katika ligi kuu ya Italia, Serie A kwa mara ya kwanza musimu huu baada ya ngoma kali baina ya viongozi wa shindano hilo ambapo, mabingwa Juventus waliwachakaza washindani wa karibu AS Roma 3-2 Jumapili.

Mechi hiyo iliyojaa uhasama ilishuhudia wachezaji wawili wakipewa kadi nyekundu, mwalimu wa Roma, Rudi Garcia kufurushwa uwanjani na penalti tatu za utata kupeana, mbili kwa faida ya Juve.

Nahodha mkongwe wa Roma, Francesco Totti, 38, alizua tetesi zinazoamika na wengi nchini humo kuwa Juventus hubebwa na waamuzi kutokana na maamuzi ya refarii Gianluca Rocchi.

“Juventus wanastahili shindano lao pekee kwani wanafanikiwa kushinda kila wakati,” Totti alisema baada ya mechi hiyo iliyoitwa ya ‘maajabu’ na nahodha mwenzake na mlinda lango wa Juvetus, Gianluigi Buffon.


Mabingwa hao wenye wafuasi wengi kutoka tumbo la Italia hadi Uswisi ndio klabu kilicho pambwa mara mingi zaidi nchinu humo na mataji 30 ya Serie A lakini wanachukiwa zaidi kufuatia tuhuma za kupendelewa na waamuzi.

Ingawa rekodi rasmi zinaonesha wameshinda mataji 30, mashabiki wao wanashikilia idadi hiyo ni 32 baada ya kupokonywa mawili kufuatia kashfa ya ‘Calciopoli’ iliyowahusisha na kupanga matokeo ya mechi kilaghai mwongo mmoja uliopita.

Licha ya ushindi huo uliofungua mwanya wa alama tatu mbele ya Roma, vyombo vya habari vilikashifu kazi ya Rocchi.