come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WENGER KUEPUKA MASHITAKA

Arsene Wenger & Jose Mourinho 

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, hatachukuliwa hatua za kinidhamu kutoka shirikisho la kandanda la Uingereza, FA, kufuatia makabiliano yake na mpizani wake Jose Mourinho wa Chelsea kwenye mechi yao ya Premier ya Jumapili.

Kulingana na ripoti iliyochapishwa na wanahabari wa Press Association, shirkisho halitafuatilia kisa hicho kwani refarii aliweza kulitatutua kulingana na mamlaka yake kilipotokea.

FA wanaweza fungua mshataka ikiwa mwamuzi ataandika kwenye taarifa yake kitendo kisicho cha kawaida baada ya Wenger kuvamia eneo la kiufundi la Chelsea na kumsukuma Mourinho wakati mchezaji wake Alexis Sanchez alifyekwa na beki Gary Cahill katika kipindi cha kwanza.


Waalimu hao walitenganishwa na afisa wan ne, Jon Moss, kabla ya kuitwa na refa Martin Atkinson ambaye aliwakemea na kuwaonya makabiliano zaidi yangepelekea kadi nyekundu.

Shirikisho hilo litaandikia timu hizo mbili baada ya mechi hiyo kucheleweshwa na dakika 15 pale mashabiki wa Arsenal walipoachilia fataki iliyojaza moshi kwenye milango ya kuingia ugani Stamford Bridge.

Maafisa wa usalama walifunga eneo hilo hadi pale moshi huo ulipoisha.