![]() |
|
|
|
Bao lake Sergio Aguero lilitosha mabingwa wa ligi
ya Premier ya Uingereza, Manchester City kuwalaza watanashari majirani
Manchester United 1-0 kwenye ngoma ya kuvutia ugani Etihad Jumapili.
Matokeo hayo yalihukumu meneja wa United, Louis Van Gaal, kupoteza kivumbi chake cha kwanza baina ya maadui hao wa jadi baada ya kumiliki utawala wa Old Trafford kabla ya mwanzo wa musimu huu.
Timu yake ilipungukiwa na mchezaji mmoja kutoka dakika ya 39 wakati beki Chris Smalling alifurushwa uwanjani baada ya kupata kadi mbili za njano katika kipindi cha dakika mbili kwa makosa ya kitoto.
City walibaki na gadhabu baada ya maombi kadhaa ya penalti kupuuziliwa na refarii Michael Oliver lakini walipata zawadi bidii zao zilistahili pale Aguero alipotia kizimbani dakika ya 63 kwa ustadi mkubwa baada ya Yaya Toure na Gael Clichy kubadilishana pasi za mpwito kumuunganishia straika huyo hatari.
Bao hilo lilimpeleka mbele ya mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa, kwenye daftari ya viongozi wa mabao na 10, goli moja mbele ya mshindani wake wa karibu.
Golikipa Joe Hart aliokoa mkwaju wake kiungo machachari Angel Di Maria ikisalia dakika 14 muda wa kawaida kukatika kunyima United nafasi ya kusawazisha kabla ya Maroune Fellaini kutupa fursa ya kutinga kwa kichwa.
City walisonga hadi alama sita nyuma ya viongozi Chelsea kusalia nafasi ya tatu kwenye daftari ya Premier huku United wakichuka hadi tisa pointi 13 nyuma ya viongozi baada ya kulazwa kwa mara ya tatu musimu huu.