come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

FELLAINI SI MTU WA KUTEMEANA MATE- LVG

Marouane Fellaini 

Louis Van Gaal amemtetea Marouane Fellaini dhidi ya madai kwamba kiungo huyo wa kati wa Manchester United kutoka Ubelgiji alimtemea mate Sergio Aguero wa Manchester City wakati wa debi iliyochezewa Etihad Jumapili.

Mitandao ya kijamii iliwaka, mjadala mkuu ukiwa iwapo video ya kisa kilichotokea kipindi cha kwanza ambapo Fellaini alisimama kando ya Aguero aliyekuwa ameanguka, na kumshutumu kwa kujiangusha, pia ilionyesha akimtemea mate straika huyo wa Argentina, aliyeshindia City 1-0.

Hata hivyo meneja wa United Van Gaal alisisitiza Fellaini si mtu wa “kutemeana mate” na wanaotazama video hiyo wameona tu ishara za hasira kutoka wka mchezaji huyo.

Fellaini bila shaka alikuwa ameghadhabishwa na kuanguka kwa Aguero eneo la hatari, na alimgeukia na kumkaripia baada ya refa Michael Oliver kukataa ombi la straika huyo la kutaka penalti.


"Nimesikia kwamba hilo linajadiliwa mitandao ya kijamii lakini tayari iwapo (Fellaini) anasema kwa sauti na wakati ukisema kwa sauti, kuna – mnayaitaje, mate? – pamoja. Sidhani yeye ni mtu wa kutemeana mate,” akasema Van Gaal.