|
|
Nyota Alexis Sanchez aling’aa tena, akifunga
mabao mawili na kusaidia ufungaji wa bao moja, na kusaidia Arsenal kutua
nambari tano ligini kwa ushindi wa 3-0 Ligi ya Premia dhidi ya Stoke
City Jumapili.
Baada ya Laurent Koscielny kuweka Arsenal kifua mbele dakika ya sita kwa bao la kichwa lililotoka kwa krosi ya Sanchez, Mchile huyo alitumia ustadi mkubwa kufunga la pili kabla ya kumaliza kazi kwa frikiki iliyopinduliwa, likiwa bao lake la 18 katika mashindano yote msimu huu.
Ushindi wa Arsenal ulitiwa ila na kuumia bega kwa difenda wao Mathieu Debuchy lakini Gunners waliweza kukaribisha tena mshindi wa Kombe la Dunia Mesut Ozil baada yake kukaa nje muda mrefu kutokana na jeraha.
Ushindi uliwezesha Arsenal kupita wapinzani wao Tottenham Hotspur na kutua nambari tano, wakiwa sawa kwa alama na Southampton ambao baadaye waliponyoka kwa kulaza Manchester United baadaye Jumapili. Kabla ya mechi hiyo, United walikuwa alama moja na nambari moja juu yao Saints.
“Ilikuwa muhimu sana kuanza mechi hiyo vyema. Tunakumbuka mechi yetu Stoke, ambapo baada ya sekunde 20 tulifungwa,” Koscielny aliambia Sky Sports.
"Tulikuwa makini sana na ni muhimu sana kufunga bao (la mapema) na muhimu zaidi kwamba tulibeba alama zote tatu.”
Timu hizo zilipokutana mechi ya kwanza Britannia Stadium Desemba Arsenal Walijipata nyuma baada ya sekunde 20 pekee na walikuwa nyuma 3-0 kufikia muda wa mapumziko lakini Jumapili Gunners walikuwa moto sana. Baada ya kunyimwa bao mara mbili na ustadi wa Asmir Begovic, Koscielny alipata nafasi kubwa eneo la hatari la Stoke na akafunga kwa kichwa krosi murua ya Sanchez.
Mwanzo mwema wa Arsenal ulitiwa ila na kuumia kwa difenda Mfaransa Debuchy aliyeondolewa uwanjani kwa machela dakika ya 13 baada yake kugongana na Marko Arnautovic.
Sanchez, nyota wa Arsenal msimu huu, aliongeza la pili kwa ustadi mkubwa karibu na mlingoti wa goli baada ya kushirikiana na Tomas Rosicky.
Stoke waliimarika mapumziko yakikaribia huku Peter Crouch akituma nje mpira wa kichwa na kumfanyisha kazi, ya kawaida hata hivyo, kipa David Ospina, aliyekuwa akianza mechi yake ya kwanza wavuni badala ya Wojciech Szczesny.
Sanchez aliongeza lake la pili na la Arsenal la tatu baada ya mapumziko kwa frikiki ya kupinduliwa ambayo ilimhepa kipa Begovic.
Santi Cazorla aligonga mwamba wa goli kwa kombora kali kabla ya bao la Geoff Cameron wa Stoke kukataliwa kwa kuotea, uamuzi fasaha kutoka kwa refa.
Nguvu mpya Ozil alituma kombora juu na nje kutoka kwa pahala pagumu kabla ya Theo Walcott, mchezaji mwingine aliyerudi baada ya kukaa nje muda mrefu kutokana na jeraha, kupoteza nafasi murua ya kufunga kwa kutoa kombora hafifu.