Timu ya Taifa ya
Tanzania(Taifa Stars) imesonga mbele katika michezo ya raundi ya kwanza
kwa kanda ya Afrika ya mchujo wa kombe la dunia litakalofanyia huko
nchini Urusi mwaka 2018.
Taifa stars wakicheza ugenini huko nchini
Malawi walikubali kulala kwa kichapo cha bao1-0 dhidi ya wenyeji wao
timu ya taifa ya Malawi The Flames.
Bao lao pekee la mchezo huo lilifungwa katika dakia ya 41 na mchezaji Dave Banda.
Licha
ya kuchapwa kwa bao hilo Tanzania wamesonga mbele kwa hatua ya pili
baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika
Jijini Dar es salaam.
Stars watacheza Raundi ya Pili na timu ya
taifa ya Algeria, ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake
zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko
Algiers hapo Novemba 17.
Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa
kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi
wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja