come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Djokovic, Muruguza wababe China Open


Image copyrightGetty
Image captionMcheza tenisi namba moja kwa ubora Novak djokovic
Mcheza tenesi namba moja kwa ubora kwa upande wa wanaume Novak Djokovic ametwaa taji la michuano ya wazi ya China.
Djokovic alimshinda Rafael Nadal anayeshikilia nafasi ya nane kwa ubora wa mchezo huo duniani kwa
Seti 6-2 6-2 na kushinda taji lake la sita kwa mwaka huu.
Na kwa upande wa wanawake Muhispani Garbine Muguruza alipata ushindi wa seti 7-5 6-4 dhidi ya Timea Bacsinszky na kutwaa taji la pili.

Kwa ushindi huo Muguruza anapanda mapka nafasi ya nne kwa ubora wa viwango vya mchezo huo.