come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA WASHITUKIA JANJA YA AZAM FC KWA MGAMBO

Na Mwandishi Wetu, Tanga

Mabingwa watetezi wa ligi kuu bara Yanga SC imeshitukia mpango wa vinara wa ligi hiyo Azam FC kutaka kuihujumu tena itakapokutana na Mgambo JKT kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga Jumamosi ya Desemba 12.

Taarifa kutoka Tanga ambapo Yanga inataraji kuwasili kwa ajili ya kuivaa Mgambo, kumebainika kulikuwa na mbinu za chinichini kutaka Yanga ipoteze mchezo huo ili wao (Azam) waendelee kushikilia usukani wa ligi, Yanga kwa kutumia makomandoo wake wameushitukia mchezo huo na wamejipanga kushinda mechi hiyo.

Azam FC inashuka dimbani siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na Simba SC ambapo wamepania kuibuka na ushindi ili waendelee kung'ang'ania kiti cha uongozi, mpaka sasa Azam FC ina pointi 25 huku mabingwa watetezi Yanga watakaoshuka dimbani siku hyo hiyo ya jumamosi wana pointi 23.


Ikumbukwe ligi ya msimu wa 2013/14 Azam FC ilitwaa ubingwa wa bara lakini ikiifanyia vitimbi Yanga ambapo ilipocheza na Mgambo JKT jijini Tanga ikafungwa 2-0 na kupoteza ubingwa