Na. Elias John, PEMBA
MABINGWA wa soka wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC wanaendelea vizuri, na kambi yao katika kujiandaa na mchezo wao wa ligi ya mabingwa barani Afrika Kati yao na AL Ahly ya Misri utakaofanyika Jumamosi ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Akizungumza na Staa wa leo mjini hapa, kocha msaidizi wa mabingwa hao Juma Mwambusi amesema wachezaji wake
wamempa matumaini ya ushindi katika mchezo hip.
Mwambusi amedai kuwa zile kasoro zilizoonekana katika machi zilizopita dhidi ya Ndanda Kagera Sugar hazitajitokeza tena.