Na Elias John, Dar es salaam
Mtangazaji mwenye Sauti Matata bongo Gardner G Habash Amerejea katika kituo cha zamani cha Clouds fm ambacho awali alikihama kwa muda.
Gardner aliyewahi kutamba na kipindi cha Jahazi amesema aliamua kupumzika utangazaji ili apate nafasi ya kufanya mambo mengine.
Aidha Habash ameongeza kuwa japo aliamua kupumzika utangazaji ili afanye mambo mengine alilazimika kuingia tena mzigoni katika vituo vingine vya Radio kutokana na dau nono alilotangaziwa na matajiri wake hasa ukizingatia muda wa kurejea Clouds fm ulikuwa haujafika.
Gardner ameendelea kufunguka kuwa kutokana na mazingira aliyokuwa anaishi huko alikotoka imemuwia vigumu hata kupanga sentensi za kuwaaga wafanyakazi wenzake jambo lililomfanya amtume mtu kabla ya yeye mwenyewe kufanya hivyo.
Amesema kwa sasa amerejea rasmi Clouds fm na kwamba mashabiki wake Watarajie mambo mazuri na Matamu kutoka Kwake na Panapo Majaaliwa ya Mwenyezi Mungu tarehe 11 mwezi Ataanza kusikika hewani.