Na Elias John, Pemba
MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania
Bara Yanga wako katika Hali nzuri kukabiliana na Al Ahly ya Misri katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika utakaofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iinayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Bara, imejidhatiti lpasavyo kukabiliana na Mafarao hao wa Misri ambao katika siku za hivi Karibuni wameonekana kushuka kiwango cha uchezaji.
Katika kambi yao iliyopo hapa Pemba kulekea mchezo huo, Yanga imerekebisha makosa yote katika kikosi chao na kwamba kinachosubiriwa kwa sasa ni mchezo huo.
Katika hatua nyingine kocha msaidizi wa wanajangwani hao Juma Mwambusi amesema kikosi chake Kipo imara na kuwaomba mashabiki wote nchi nzima kuhudhuria kwa wingi katika mchezo ili Kuwapa hamasa wachezaji wake.