Na Johnson January, Dar es salaam.
WAKATI presha ikiwa Juu kwa wanajangwani kuhusiana na mtanange wa na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika, mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro, amewatoa hofu mashabiki wake kuwa mchezo huo utarushwa hewani moja kwa moja (live) na kituo cha runinga cha Azam TV.
Muro ameyasema hayo Jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine Muro amewahakikishia wanayanga kuwa katika mchezo huo ushindi hauna mjadala.
Yanga itamenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri siku ya Jumamosi katika uwanja Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo unaotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki lukuki.