Na mwandishi wetu.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi mwenye asili ya Kongo Ndanda Kosovo, amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kosovo ni Mingoni mwa waanzilishi kundi la muziki wa dansi ambalo miaka kadhaa lilivuma sana na wimbo ujulikanao kwa Jina la Binadamu.
Ndanda amejizolea umaarufu mkubwa Kutokana na sauti yake ya zege iliyokuwa inakonga vilivyo nyoyo za mashabiki wake.
Ndanda alilazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda kadhaa akipigania matibabu na kufikia mapema ya leo Mwenyezi Mungu kaichukua roho yake.
Mtandao wa Staa wa leo, unawapa pole ndugu ndugu na jamaa wote waliofikwa na msiba huo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi Amina.