come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

#MICHEZO: TUTAWAONYESHA HUKO HUKO KWAO: WASEMA YANGA

Na Elias John, jangwani.

LICHA ya jana kulazimishwa kutoka sare ya 1-1 na timu ya Al Ahly ya Misri tena katika uwanja wa nyumbani,  mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC wamesema watafanya kile kisichotarajiwa na wengi.

Wamesema mpira hauna nyumbani wala ugenini ila wamesema mpira una matokeo matatu tu ambayo ni sare, kufungwa na kufunga na ndio maana japo Al Ahly walikuwa ugenini lakini wameweza kupata sare.

Wameongeza kuwa katika mchezo huo wa marudiano watafanya kila wawezavyo ili wapate goli la mapema ili wajiweke katika nafasi nzuri.

Wamesema kwamba wanakua mchezo utakuwa na tension kubwa ila hiyo haitawasumbua kwani wamejipanga kuleta raha kwa watanzania.

Katika mchezo wa jana Al Ahly walikuwa ndio wa kwanza kujipatia goli ambapo mnamo dakika ya 11 tu ya mchezo Al Ahly waliweza kuliona lango la Yanga kupitia kwa mshambuliaji wao Gamel na mnamo dakika ya 19 ya mchezo katika harakati za kuokoa hatari katika lango lake beki kisiki wa timu hiyo ajulikanae kwa Jina la Ahmed amejikuta akiutumbukiza mpira kimiani katika lango lake hivyo kufanya matokeo hadi mwisho wa mchezo kuwa sare ya 1-1.