come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Masikini Crazy Buffa

Na Poul Mokiwa

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Kharid Yusuph au Crazy Buffan inasemekana yuko hoi bin taaban kufuatia kupatwa na maradhi ya miguu na kushindwa kutembea.
 Akizungumza na mwandishi wa Kabumbu Spoti, Rafiki wa msanii huyo Fikiri Salum amesema kuwa Buffa anaumwa sana na anashindwa hata kutembea, Fikiri ameongeza kuwa tangia mwanam,uziki huyo apatwe na maradhi hayo anashindwa hata kukaa na amebakia kuugulia maumivu.

Timu ya Kabumbu ilifanikiwa kukutana na nyota huyo aliyepata kutamba na wimbo wa Ukibebwa Jishikie ambao alimshirikisha Mkali mwenzake Banana Zorro.

Buffa amedai alianza kuumwa yapata mwezi sasa na ameshindwa kwenda kazini kwake, 'Yaani naumwa sana tena inayosumbua zaidi ni miguu na maeneo ya kiunoni', alisema Buffa.

Msanii huyo ameongeza kuwa hakuwahi kuugua maradhi hayo ila ndio kwanza yameanza kumsumbua sasa, Anaongeza kuwa amejaribu kwenda hospitali kadhaa lakini wameshindwa kugundua kinachomsumbua, Hivi karibuni nyota huyo alikwenda hospitali inayomilikiwa na Wachina ambapo alipatiwa dawa ambazo anaendelea nazo lkakini anasema bado hajapata nafuu.

Buffa amewataka mashabiki wake kumuombea ili apone haraka na aendelee na shugjhuri zake za kila siku, Msanii huyo aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo ile ya Friday Night aliyoshirikishwa na mkali wa TAKEU Mr Nice