Katika mchezo huo uliohudhuriwa na washabiki wengi wa soka kutoka mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya jirani, umeishia kwa sare hiyo ya pasipo kufungana huku mwamuzi wa mchezo huo Dominic Nyamisana na wasaidizi wake wakishindwa kulimudu pambano hilo kutokana na kutokua makini.
Watoto wa jangwani waliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kupata bao la mapema na katika dakika ya tatu mchezo, Hamis Kiiza alishindwa kuipatia Yanga bao la kuongoza kutokana na kutokua makini katika umaliziaji.
Polisi nayo ilijaribu kufanya mashambulizi ya kushtukiza lakini umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa kikwazo kwao kuweza kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'
Yanga iliendelea kufanya mashambulizi langoni mwa timu ya Polisi lakini kutokua makini kwa washambuliaji wa Yanga Saimon Msuva, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza na Nizar Khalfani ulishindwa kuipatia Yanga bao .
Mpaka mpira unakwenda mapumziko, wenyeji Polisi Morogoro 0 - 0 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Stephano Mwasika aliyechukua nafasi ya Nizar Khalfani, mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa timu ya Yanga ambapo iliweza kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Polisi.
Baada ya Yanga kuwa inafanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Polisi na kusababisha kupata kona nyingi mfululizo, wachezaji wa Polisi waliamua kuwa wanajiangusha kila dakika ili kupoza kasi ya mchezo huku mwamuzi akionekana kutokujali kwa tabia hiyo ya wachezaji.
Polisi waliendelea kucheza kwa kupoteza muda hali iliyopelekea kupoteza radha ya mchezo, dakika za majeruhi Yanga ilifanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Polisi lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuipatia bao.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Polisi Morogoro 0 - 0 Young Africans.
Kwa matokeo hayo ya leo Young Africans inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kufikisha pointi 49 ikiwa ni pointi 6 mbele ya timu ya Azam inayokamata nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 43.
Kikosi cha Young Africans: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Frandk Domayo, 9.Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu, 10.Hamis Kiiza, 11.Nizar Khalfani/Stephano Mwasika