MSHAMBULIAJI wa Napoli, Edinson Cavani amewapiga stop wazazi wake kuzungumzia mustakabali wake kwenye umma.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 26 wa Uruguay, alikuwa tayari amehusishwa na
mpango wa kuhamia Manchester City, kabla ya mama yake kusema amefanya
mazungumzo na klabu zote, City na Real Madrid.
Kisha maelezo ya baba yake yakapendekeza Cavani amekubali kujiunga na Real, kwa dau la Euro Milioni 63 (Pauni Milioni 54).
Amewatolea uvivu: Cavani akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Uruguay nchini Brazil jana
Lakini
Cavani, ambaye amefunga mabao 29 katika ligi akiwa na Napoli msimu
uliopita, amewataka wazazi wake wakae kimya na wakati ukifika utatoa
majibu.
Akinukuliwa na La Repubblica, aliwaambia Waandishi wa Habari: "Baba yangu amezungumza kuhusu Real? Nataka niseme hayo maneno si yangu.
"Nimewaambia wazazi wangu mara elfu, wasizungumze tena. Wanaweza kuniumiza tu mimi.
"Mimi ni mali ya Napoli kama ilivyo na hiyo itategemea na klabu. Kama suluhisho lingine, litakuja lenyewe, tutamua.'
Rais
wa Napoli, Aurelio De Laurentiis ameripotiwa akisema mshambuliaji wake
huyo anatakiwa kufanya uamuzi juu ya mustakabali wake hadi kufikia Julai
20, akirejea kutoka kwenye Kombe la Mabara anakoiwakilisha Uruguay.
Na
alipoulizwa ikiwa Real Madrid - ambayo sasa iko chini ya kocha wa
zamani wa Chelsea na Paris Saint-Germain, Carlo Ancelotti - itakuwa
sehemu yake sahihi, Cavani alibakia kuficha.
"Nitaweka wazi juu ya hilo pia - wakati wote nimekuwa nikisema ni moja ya klabu bora duniani.
Anatisha: Nyota huyo wa Uruguay amekuwa mfungaji bora wa Serie A msimu uliopita
"Wote
tumekuwa tukiota vizuri tu kuchezea timu yao, kama ambavyo tunaota
kuhusu Barcelona, lakini sasa nipo Napoli na ninajivunia kwa kweli.
"Kama
nitaiacha nyuma jezi ya bluu siku moja, nitajiunga na klabu kubwa tu.
Wazi kuna mashabiki ambao wataelewa na wengine ambao hawataelewa.
"Lakini sitaki kuteleza nyuma ya mlango, Nataka kutoka mbele ya mlango, siku ambayo hatimaye mambo yatakuwa,"