come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

JUMA KASEJA AGEUKA MFALME MSIMBAZI, VIONGOZI WAHAHA KUMSAINISHA


Juma Kaseja
 
Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha kumtosa kipa wao chaguo la kwanza Juma Kaseja na kusisitiza kuwa bado nahodha huyo wa timu ya taifa (Taifa Stars) bado anayo nafasi ya kupewa mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaonza Agosti 24.

Kaseja aliyejiunga na Simba mwaka 2002 akitokea Moro United ya Morogoro, anamaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo Jumapili ya Juni 30 mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema kwamba suala la Kaseja bado liko mikononi mwa viongozi wa klabu hiyo na maamuzi yoyote yanaweza kufanyika ndani ya mwisho wa wiki.

Mtawala alisema kwamba kiufundi, Kaseja anakubalika lakini nje ya uwanja ndiyo kuna maneno 'yanayommaliza' kipa huyo ambaye pia ni nahodha wa klabu yao.

"Kiufundi huwezi kumuacha Kaseja kirahisi. Lakini kuna mambo mengi yanazunguka katika usajili wake na hivyo ni lazima watu wakutane na kujadiliana kwa hoja kabla ya kufikia muafaka, ila bado kikao cha mwisho hakijafanyika na hivyo binafsi siwezi kusema kama atakuwapo au hatakuwapo msimu ujao," aliongeza Mtawala.

Alisema kwamba pamoja na lawama anazopewa kipa huyo na baadhi ya mashabiki, ukweli unabaki kwamba kwa ujumla wake, bado ni kipa hodari na amekuwa akikubali kuitumikia timu hata pale ambapo hakuwa ametarajia kuanza kutokana na sababu mbalimbali zinazojitokeza kwenye kikosi.

"Tofauti na timu nyingine makipa wengi wanadaiwa kutopendana, kwa Kaseja na Dhaira wao hiyo ilikuwa tofauti, wanashauriana na kuzungumza mara kwa mara," alisema Mtawala.

Simba ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya tatu hivyo mwakani haitashiriki mashindano yoyote ya kimataifa.
Kocha wa klabu hiyo, Abdallah Kibaden 'King' aliumbia mtandao huu hili hivi karibuni kuwa si yeye aliyemtema Kaseja bali viongozi wa klabu hiyo ndiyo wanajua siri ya sababu ya kuliondoa jina la kipa huyo.