Jaji wa mahakama hiyo, Anju Deb Rani, alisema watu hao watapanda kizimbani Septemba 17.
Messi ambaye ni Mwanasoka Bora wa Dunia mara nne,
pamoja na baba yake huyo, Jorge Horacio, watafika mahakamani ikiwa ni
utaratibu wa kawaida wa mahakama kabla ya kuanza uchunguzi rasmi.
Jaji alisema malalamiko ya ukwepaji kodi
yaliwafikia na wamechukua hatua ya kuwaita watu hao mahakamani ikiwa ni
utaratibu wa kawaida wa mahakama. Alisema: “Baada ya tukio hilo,
uchunguzi wa kina utafanyika kuona kama jambo hilo ni la kweli au la.”
Juni 12 Messi alidaiwa kukwepa kodi kwa miaka mitatu kuanzia 2007 mpaka 2009.
Kama wakipatikana na hatia, wawili hao watatoa
fidia ya asilimia 150 ya kodi waliyokwepa au kifungo jela cha kati ya
miaka miwili mpaka sita.