KLABU ya Arsenal imeibuka na mpango B katika msako wake wa mshambuliaji wa kati iwapo itamkosa Luis Suarez.
The Gunners imemuweka nambari moja
mshambuliaji huyo anayetaka kuondoka Liverpool, lakini tayari ofa zao
mbili zimekwishapigwa chini na klabu ya Anfield.
Arsenal bado ina matumaini ya kushinda
sakata hilo kwa kumnsa mpachika mabao huyo tishio, ikibidi kutuma ofa ya
tatu ya Pauni Milioni 50, kiwango cha chini kinachotakiwa na Liverpool.
Kupitia Sportsmail, inafahamu kwamba The Gunners imeanza mpango wa kumpata mkali mwingine, iwapo itamkosa Suarez.
Majadiliano baina ya benchi la Ufundi na Maskauti wa klabu yamechukua nafasi siku chache zilizopita juu ya mchezaji mbadala.
Tayari, Arsenal imewakosa Gonzalo
Higuain na Stevan Jovetic ambao wote kocha Arsene Wenger alikuwa
anawahitaji sana majira haya ya joto, hivyo akahamia kwa Suarez.
Anatakiwa? Edin Dzeko, pichani mjini Munich akiwa na Manchester City, amerudi katika kiwango kwenye mechi za kujiandaa na msimu
Wengine wanaotakiwa: Stevan Jovetic (kulia) amechagua Manchester City, lakini Michu (kushoto) anabaki kwenye rada za Arsenal
Mmoja aliyeota mbawa: Gonzalo Higuain (katikati) ametimkia Napoli. Hapa akishangilia kufunga dhidi ya Benfica
Higuain ameenda Napoli na Jovetic ametua Manchester City, wakiiacha The Gunners ikisotea sani za wengine.
Wayne Rooney alikuwa anatakiwa pia
mwanzoni, wakati klabu hiyo imepokea taarifa ya Maskauti wake kuhusu
mshambuliaji wa Swansea, Michu na wa Manchester City, Edin Dzeko.
Liverpool wanasistiza hawatamuuza Suarez
kwa Arsenal kwa namna yoyote, lakini The Gunners haijabwaga manyanga
katika jaribio lake la kunasa saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
Uruguay, ambaye yu tayari kuondoka Anfield kutua Emirates.
Mchezaji pekee ambaye Arsenal ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili ni kiungo mkabajia wa Bayern Munich, Luis Gustavo.
The Gunners imeanza mazungumzo na mabingwa hao wa Ulaya juu ya ofa ya Pauni Milioni 14.5 kumnasa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil.
The Gunners imeanza mazungumzo na mabingwa hao wa Ulaya juu ya ofa ya Pauni Milioni 14.5 kumnasa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil.
Bado anasaka: Arsene Wenger (kulia), akizungumza na Manuel Pellegrini, anataka kuongeza wachezaji kikosini mwake
Na Gustavo, ambaye hana nafasi kwa sasa
katika kikosi cha kwanza Allianz Arena, yupo tayari kuhamia London, na
amesema: "Wao [Arsenal] ni timu kubwa na ambayo itakuwa ni nafasi kubwa.
"Nataka kwenda klabu ambayo nitacheza,".
Wakati huo huo, Malaga inataka kumtumia beki wa kulia, Jesus Gamez kama
sehemu ya majadiliano ya kumsaini Nicklas Bendtner.
Arsenal inataka kusaini beki mpya wa
kulia awe msaidizi wa Bacary Sagna, ambaye anaweza kutumika katika beki
ya kati mwanzoni mwa msimu kutokana na Thomas Vermaelen kuwa majeruhi.
Na Malaga inataka kumtumia Gamez, mwenye umri wa miaka 28, kama sehemu ya dili lao na Gunners kwa Bendtner.
Anayetoka na Anayeingia: Luiz Gustavo (kushoto) anaweza kutua akitokea Bayern Munich wakati Nicklas Bendtner anataka kuondka